Jaji Mkuu ashauri Polisi kuacha kutangaza taarifa dawa za kulevya



Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma akizungumza na watumishi katika ofisi ya mahakama ya Wilaya ya Pangani wakati wa ziara yake wilyani humo.
Pangani. Hatua ya utangazaji wa dawa za kulevya nchini inayofanywa na maofisa  wa Jeshi la Polisi nchini  kutangaza kwa kutumia vyombo vya habari kinyume na utaratibu wa ukusanyaji ushahidi katika uendeshaji wa kesi za dawa za kulevya.

Hayo yameelezwa na Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Tanga.
Amesema katika kesi za dawa za kulevya kumekuwa na changamoto za kukamilika kwa ushahidi kutokana na ukiukwaji wa ukusanyaji wa ushahidi unaofanywa na watu kinyume na utaratibu.
'Kukamata dawa za kulevya na kuita waandishi wa habari na kutangaza ukionyesha umekamata dawa za kulevya, unakiuka utaratibu wa ukusanyaji ushahidi. Utaratibu unatakiwa kuwa baada ya kitendo cha kukamata dawa za kulevya, yanatakiwa kufungwa na kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa ajili ya uchunguzi.
"Hatua ya kukamata na kutangaza husababisha watu wanaokuwa na kesi hizo kuachiwa huru kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kujitosheleza wa kumtia hatiani kisha lawama zinakuja kwa mahakama kwamba imewaachia huru," amesema.
 Pamoja na mambo mengine, amesema kuna taratibu huwa hazifuatwi wakati wa ushahidi ambapo amesisitiza watu kuzifuata.
Aidha, Jaji Mkuu amewataka mahakimu wanapofungua mashauri kuwe na taratibu za mtu kutaja mtaa anaotoka na anuani ya makazi ili kuweza kumtambua mtu hadi mahali anapoishi .
"Natoa wito kwa Watanzania kuingia katika tovuti yetu na kujifunza masuala ya kisheria ili mtu aweze kuwa na uelewa na masuala ya kisheria na mtandao unafanya kazi saa 24," amebainisha.
Awali, akitoa taarifa za huduma za utoaji haki katika Wilaya ya Pangani, Mkuu wa Wilaya ya Pangani, Ghaibu Lingo amesema Wilaya hiyo inakabiliwa na changamoto ya uchakavu wa jengo la mahakama na uelewa mdogo wa wananchi kuhusu masuala ya kisheria.
Amesema Wilaya ya Pangani kuna tatizo la matukio ya ulawiti na ubakaji na kwamba kesi hizo huishia kumalizwa na familia kutokana ulewa mdogo jambo linalosababisha mahakama kukosa ushahidi.

"Matukio ya ulawiti na ubakaji ushahidi ni tabu kupatikana kwa sababu yanaanzia kwenye familia hivyo linapofika mahakamani ushahidi unakosena," amesema mkuu huyo wa wilaya.
Jaji Mkuu yuko ziarani mkoani Tanga kukutana na watumishi na wadau wa mahakama, kukagua majengo na matumizi ya Tehama mkoani humo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad