MWENYEKITI wa NCCR- Mageuzi, James Francis Mbatia, amedai kuwa unaoitwa, “mkutano wa Halmashauri Kuu (NEC) ya chama chake” uliomsimamisha wadhifa wake, “ni batili.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
“Hakuna mkutano wowote wa Halmashauri Kuu ya NCCR Mageuzi, uliyoitishwa na uongozi wa chama. Kamati Kuu (CC), haijawahi kuitisha mkutano na hivyo, kinachoitwa mkutano wa NEC, ni kitu ambacho siyo halali,” ameeleza Mbatia.
Amesema, atashangaa ikiwa Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi, atabariki maazimio ya mkutano huo.
Amesema, jana chama chake kilipeleka kwa msajili muhtasari wa kikao cha Kamati Kuu, ambapo pamoja na mengine, kumjulisha kusogezwa mbele kwa Mkutano wa Kamati Kuu na kumsimamisha kazi, Katibu Mkuu, Matha Chiumba.
Hata hivyo, Mbatia hakueleza MwanaHALISI anachukua hatua gani, kukabiliana na “mapinduzi hayo.”
Badala yake, mwanasiasa huyo aliishia kusema, “bado naendelea kujadiliana na wenzangu, kuona hatua za kuchukua.”
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya chama hicho, Kamati Kuu, iliyokutana mwishoni mwa wiki, iliamua kuusogeza mbele mkutano huo hadi 18 Agosti mwaka huu.
Lakini muda mfupi baadaye, Edward Simbeye, Mkuu wa Idara ya Uenezi na Mahusiano ya Umma, ametoa taarifa kuwa Mbatia na baadhi ya viongozi wenzake, watakutana kujadili hatma ya chama chao, saa nane mchana wa leo Jumamosi.
Mkutano wa NEC unaodai kumsimamisha Mbatia kwenye uongozi, ulisimamiwa na Haji Ambari, Makamu Mwenyekiti Zanzibar.
Ambari anakumbukwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba, kwa kusaliti Zanzibar baada ya kupigia kura Katiba Inayopendekezwa na hivyo, kupatikana theluthi mbili ya kura zilizokuwa zinahitajika