Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limesema limeendelea kuisimamia operesheni maalum kali na msako wa mtaa kwa mtaa dhidi ya Vijana wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu maarufu Panya Road na mpaka May 6,2022 limewakamata Wahalifu 31 kwa tuhuma za kujihusisha na matukio ya uporaji baada ya kuvunja nyumba, kujeruhi na kuiba vitu mbalimbali vya nyumbani .
"Operesheni hii ambayo ni endelevu ilianza tarehe 27/04/2022 na imefanikiwa kuwakamata Wahalifu hao ambao wengi wao ni vijana wenye umri kati ya miaka 13-20 na wakati wanafanya uhalifu wanatumia mapanga, visu, nondo, na mikasi mikubwa"
"Katika mahojiano ya kina, Jeshi la Polis limebaini kuwa Watuhumiwa hao wamehusika katika vitendo hivyo vya kihalifu na kuonesha baadhi ya vitu walivyoibwa zikiwemo TV 12 na simu za mkononi 4"
"Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatoa onyo na halitasita kuwakamata ambao wamekuwa wakipokea mali mbalimbali za wizi zinazotokana na matukio ya kihalifu na Jeshi la Polisi halitasita kuwafikisha kwenye vyombo vingine vya kisheria" Jumanne Muliro, Kamanda wa Polisi Kanda Maaalum ya DSM