Kipa Diarra Amfunika MANULA Vibaya Sana...Hii Ndio Historia Fupi ya Mafanikio yake Africa


Djigui Diarra amecheza michuano ya kombe la Dunia Under (20) hadi nusu fainali. Alidaka penati mbili kwenye robo fainali dhidi ya Germany na kuifanikisha timu yake ya taifa kutinga nusu fainali.

Amecheza fainali za (AFCON) under 23 akiwa golikipa namba moja. Kwenye tuzo za (CAF) 2015, Djigui Diarra aliorodheshwa kwenye tano (5) bora ya magolikipa bora chipukizi barani Afrika.

Diarra amecheza fainali za (CHAN) mara mbili kwenye Senior team akiwa golikipa namba moja wa Mali Katika fainali hizo za (CHAN) mwaka (2016).

Diarra aliisaidia timu yake ya Mali kutinga fainali,, Walipoteza dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo kwenye fainali hiyo. Diarra aliorodheshwa kuwa golikipa bora namba (2) Afrika mwaka (2016).

Diarra alidaka penati (3) katika mechi (6) kwenye michuano hiyo ya CHAN.

Mwaka (2020) Djigui Diarra allisaidia tena timu yake ya taifa ya Mali kutinga tena fainali ya CHAN,, Katika michuano hiyo aliweka rekodi ya kucheza dakika (365') bila kuruhusu goli kwenye nyavu zake, ikiwemo kudaka penati muhimu hatua ya nusu fainali Vs Guinea

Diarra alifika hatua ya (16) bora kwenye michuano ya AFCON mwaka 2019, alicheza mechi zote kwa dakika (90') Alifungwa goli (1) na timu ya taifa ya Ivorycoast goli la Wilfred Zaha.

Mwaka (2016) Diarra alichaguliwa kwenye kikosi bora cha (CAF) Huyo ndiye Djigui Diarra, sio kwamba ubora alionao ameanzia Yanga kuuonesha, ni golikipa bora hata kwenye michuano mikubwa ya kimataifa tangu zamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad