Kipigo cha Yanga ndo Hivyo Tena..Huenda Simba Wakampiga Kocha Chini



KIPIGO cha bao 1-0 kilichoing’oa Simba katika michuano iliyokuwa tegemeo pekee kwa timu hiyo kubeba taji msimu huu, imemuweka kwenye wakati mgumu kocha Pablo Franco ambaye kwa sasa anahesabiwa saa ndani ya klabu hiyo.

Habari za ndani zinasema, huenda mabosi wa Simba wakatangaza kumpiga chini ,Pablo leo Jumatatu watakapotoa tamko lao kutokana na matokeo ya mechi yao ya juzi dhidi ya Yanga katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la ASFC, iliyopigwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Pablo ambaye ameshindwa kuuridhisha uongozi wa Simba kutokana na matokeo mabovu tangu kujiunga akitokea Hispania, alipewa mechi moja tu dhidi ya Yanga kama atafungwa hatakuwa na maisha marefu Msimbazi jambo ambalo limemshinda huenda leo akafungashiwa virago.

Awali chanzo cha kuaminika ndani ya Simba kililithibitishia Mwanaspoti kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Barbara Gonzalenz alifanya mazungumzo na meneja wa Pablo akimlalamikia kuwa hawaridhishwi na kiwango cha kocha huyo na kumpa mchezo mmoja dhidi ya Yanga.


Kabla ya mchezo huo uongozi wa Simba na benchi la ufundi walikuwa na kikao maalum ambacho kilitumia zaidi ya masaa mawili kumjadili kocha na kumtaka kuhakikisha anafanya vizuri kwenye mchezo wa nusu fainali Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) ili kupata nafasi ya kutetea taji moja lakini imeshindikana.

Mwanaspoti lilifanya jitihada za kuwasaka viongozi kuzungumzia hatma ya Pablo baada ya kukosa matokeo mazuri na mipango yao baada ya kulitema taji moja alisema watakutana leo kujadili mustakabali wake pamoja na watakavyokamilisha msimu na hali ya majeruhi waliyonayo.

“Sio rahisi kuwa na jibu la moja kwa moja leo kuhusu kocha nafikiri Leo (Jumatatu) kutakuwa na kikao kuhusu mustakabali wa timu na kufanyia kazi kauli ya Rais wa Heshima Mohamed Dewji ‘Mo’ ambaye ameitaka bodi kukaa na kufanya maamuzi magumu hili sio la kukurupuka ni la kukutana na kufikia maamuzi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad