Kiungo Fundi Said Ntibanzokiza ‘Saido’ Apewa Mkataba Mgumu Yanga, Abanwa Kuondoka




Kiungo mshambuliaji mkongwe Mrundi, Said Ntibanzokiza ‘Saido’.
KIUNGO mshambuliaji mkongwe Mrundi, Said Ntibanzokiza ‘Saido’, amepewa mkataba wa mwaka mmoja wenye masharti magumu katika Klabu ya Yanga.

Mrundi huyo ambaye anasubiria utambulisho hivi sasa, juzi aliongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuichezea timu hiyo utakaomalizika 2023.

Saido ni kati ya wachezaji ambao mikataba yao ilikuwa inatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu akiwa na wengine baadhi Dickson Job, Bakari Mwamnyeto, Yacouba Songne na Kibwana Shomari ambaye tayari ametambulishwa na timu hiyo, baada ya kuongeza miaka miwili.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, katika mkataba wa mwaka mmoja ambao ameusaini Saido, kuna kipengele kinambana kiungo huyo kuondoka Yanga.


 
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kipengele hicho ni cha kuongeza mkataba mwingine mpya katika timu hiyo, mara baada ya mwaka mmoja kumalizika kama uongozi ukiridhishwa na kiwango chake.

Aliongeza kuwa lengo la kumuongezea mkataba huo ni kumbana kuondoka katika timu hiyo ambayo katika msimu ujao itacheza michuano ya kimataifa.

“Saido ameongezewa kipengele kigumu katika mkataba wake mpya wa mwaka mmoja ambao ameuongeza Yanga ambao unamzuia kuondoka kwenda popote kama klabu ikimhitaji.

“Katika mkataba huo kuna kipengele cha kuongeza mkataba mwingine mpya mara baada ya huo alionao kufikia kikomo mwaka 2023 ambao ndiyo unamalizika.

“Kipengele hicho kitamfanya Saido kuwepo Yanga kwa muda mrefu na katika makubaliano hayo, Saido ataongezewa mkataba mwingine wa kuendelea kubakia kutokana na kiwango bora ambacho atakuwa amekionyesha,” alisema mtoa taarifa huyo.

Akizungumzia hilo, Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela alisema: “Mkataba ni siri kati ya mchezaji na viongozi, hivyo ngumu kwangu kuweka wazi makubaliano tuliyokubaliana na mchezaji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad