Kocha Pablo: Tulibahatisha kumchezesha Chama, Sakho

 


Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC Franco Pablo Martin amefichua siri ya uwezo wa Viungo Clatous Chotta Chama na Pappe Ousman Sakho, baada ya kuwatumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Young Africans jana Jumapili (April 30).


Miamba hiyo ya Soka la Bongo ilikutana Uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa Mzunguuko wa 21 wa Ligi hiyo, na kuambulia sare ya bila kufungana.


Kocha Pablo amesema aliwatumia wachezaji hao kama kubahatisha, lakini ukweli ni kwamba hawakuwa katika kiwango cha kawaida, kama ilivyozoeleka na Mashabiki wengi wa Soka la Bongo.


Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema anaamini mchezo wowote unaokutana na mpinzani wako mkubwa, unapaswa kuwa na wachezaji wenye hadhi na kiwango cha hali ya juu, lakini kwa wachezaji wake hao kutoka nje ya Tanzania hawakuwa timamu kimwili.


“Hata kama una kipaji (fundi), kwenye mechi kama hizi unahitaji kuwa fiti 200% pindi unapokutana na mpinzani mnayekaribiana uwezo. Tulijua hawako fiti lakini tulicheza kamari, nilipoona hawaoneshi utofauti, ilibidi tuwapumzishe.” Amesema Kocha Pablo


Chama raia wa Zambia alilazimika kupumzishwa baada ya kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Kiungo mwenzake Rally Bwalya, huku Sakho raia wa Senegal akitolewa dakika ya 86 na nafasi yake ikajazwa na Mshambuliaji John Bocco. Kwa matokeo ya sare ya 0-0, Simba SC inaendelea kukaa nafasi ya pili kwa tofauti ya alama 13, ikifisha alama 42, huku Young Africans ikisalia kileleni kwa kufikisha alama 55.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad