Kocha Simba Ashtukia Dili Simba Abadili Mbinu Kuhakikisha Kikosi Kinarudisha Furaha



 

KOCHA Mkuu wa Simba SC, Pablo Franco, ameamua kubadili mbinu kuhakikisha kikosi chake kinarudisha furaha kwa mashabiki na kumaliza msimu vizuri, huku akianza jambo hilo katika mchezo wa leo Jumapili dhidi ya Ruvu Shooting utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Katika hilo, Pablo ameamua kuunda vikosi viwili ambavyo vitakuwa na uwezo wa kucheza mechi kulingana na aina ya uwanja wanaokwenda kuuchezea.

 

Simba imekuwa na wakati mgumu zaidi msimu huu katika kutetea taji lake la Ligi Kuu Bara ikiwa imeachwa pointi 13 na vinara Yanga, huku ikibakiwa na mechi tisa. Yanga inazo nane.

 

Kitendo cha Simba kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Namungo hivi karibuni, mechi ikichezwa Uwanja wa Ilulu, Lindi, ndicho kimemfanya Pablo kushtuka zaidi.


Kikosi cha Simba.

Kabla ya hapo, Simba mechi tano za ugenini nje ya Dar katika Ligi Kuu Bara ilizocheza hivi karibuni, imeshinda moja (Coastal Union 1-2), ikipoteza mbili (Mbeya City 1-0, Kagera Sugar 1-0) na sare mbili (Mtibwa 0-0 na Polisi Tanzania 0-0).

 

Chanzo chetu kutoka Kambi ya Simba iliyopo Mbweni, Dar, kimeliambia Spoti Xtra kwamba: “Kocha ameigawa timu ili kuona anakabiliana na hali ya viwanja ilivyo, anasema kuna wachezaji wameshachoka kutokana na michezo mfululizo iliyopita, ila pia kuna baadhi wanaonekana kutohimili hali ya viwanja vibovu vya mikoani ndiyo maana sasa ameamua kubadili mbinu.

 

“Amesema amekuwa akiangalia kwa muda suala hilo, hivyo tayari ameamua kulifanyia ufumbuzi ili kuhakikisha hatoi nafasi kubwa ya kupoteza au kuruhusu sare mechi zijazo za mkoani.”

 

CHAMA, KANOUTE MAJANGA

Leo Jumapili Simba ikitarajiwa kucheza dhidi ya Ruvu Shooting, inatarajiwa kuwakosa Clatous Chama na Sadio Kanoute ambao ni majeruhi.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Tuna majeruhi wawili ambao hawatacheza mechi ya kesho (leo) ambao ni Sadio Kanoute na Clatous Chama.”

 

MASAU BWIRE ATAMBA

Kwa upande wa Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, kuhusu mchezo huo wa leo, amesema: “Watu nilipowaambia nakwenda kuifunga Yanga walihisi natania na badala yake waliona nini kilitokea, leo pia nasema tunakwenda kutafuta ushindi mbele ya Simba.

 

“Baada ya mchezo kumalizika watu ndiyo wataelewa nini nilikuwa namaanisha, lakini kwa sasa wanaweza wasielewe nini nazungumza.

 

“Hatuangalii kwa kuwa tutacheza na Simba basi tutaogopa jina lao, tunahitaji ushindi ili tujiweke sehemu nzuri kwenye msimamo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad