Korea Kaskazini yatangaza kifo cha kwanza kutokana na Covid-19



Maelezo ya picha, Inaaminika hii ni mara ya kwanza kwa Kim Jon- un kuonekana na barako
Korea Kaskazini imethibitisha kifo chake cha kwanza kutokana na Covid-19, huku vyombo vya habari vya serikali vikiongeza kuwa makumi ya maelfu zaidi wanaugua dalili za homa hiyo.

Watu sita walifariki baada ya kuugua homa huku mmoja akipatikana na virusi vya Omicron, vyombo vya habari vya serikali viliripoti Ijumaa.

Ilisema watu 187,000 walio na homa walikuwa "wakitengwa na kutibiwa".

Wakati wataalam wanaamini kuwa virusi hivyo vimekuwepo nchini kwa muda mrefu, viongozi walitangaza kesi za kwanza siku ya Alhamisi.

Walisema kumekuwa na kuzuka kwa virusi vya Omicron katika mji mkuu, Pyongyang, na kutangaza hatua za kutotoka nje. Hawakutoa nambari sahihi za visa hivyo.

Lakini katika sasisho siku ya Ijumaa, shirika rasmi la habari la KCNA liliripoti kwamba mlipuko huo ulienea zaidi katika mji mkuu.

"Homa ambayo sababu yake haikuweza kutambuliwa ilienea kote nchini kutoka mwishoni mwa Aprili," ilisema.


Maelezo ya picha, Bw Kim alifanya mkutano siku ya Alhamisi kujadilia hali ya Covid nchini humo.
Takriban watu 350,000 walikuwa wameonyesha dalili za homa hiyo, iliongeza, bila kutaja ni wangapi wamepima virusi vya Covid.

Picha iliyotolewa na vyombo vya habari vya serikali ilionyesha maafisa - wote wamevaa barakoa wakikutana na Kim Jong-un kujadili Covid-19

Wachambuzi wanapendekeza takwimu za hivi punde kutoka kwa vyombo vya habari vya serikali, ikiwa ni pamoja na kukiri kwamba homa isiyojulikana ilikuwa imeenea kote nchini, inaweza kuashiria nchi inakabiliwa na milipuko tofauti na ambayo imeona hadi sasa.

Idadi ya wakazi wake milioni 25 wako hatarini kutokana na ukosefu wa mpango wa chanjo na huduma duni za afya, wataalam wanasema.

Korea Kaskazini ilikataa msaada kutoka kwa jumuiya ya kimataifa ya kusambaziwa mamilioni chanjo za AstraZeneca zilizotengenezwa China mwaka jana.

Badala yake, ilidai ilikuwa imedhibiti Covid kwa kufunga mipaka yake mapema Januari 2020.

Nchi hiyo inashiriki mipaka ya ardhi na Korea Kusini na Uchina, ambazo zote zimepambana na milipuko. Uchina sasa inajitahidi kupambana na wimbi la Omicron na kufunga mipaka katika miji yake mikubwa.

Siku ya Ijumaa, KCNA iliripoti kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alikuwa ametembelea kituo cha afya na "kujifunza kuhusu kuenea kwa Covid-19 kote nchini".

Ilielezea hali hiyo kama "tatizo la kutatuliwa haraka la afya ya umma".

Katika mkutano ulioangazia sheria mpya za Covid mnamo Alhamisi, Bw Kim alionekana amevaa barakoa kwenye runinga kwa kile kinachoaminika kuwa mara ya kwanza.

Aliamuru udhibiti wa virusi vya "dharura ya juu", ambayo ilionekana kujumuisha maagizo ya kutotoka nje na vizuizi vya kukusanyika mahali pa kazi.

Kuna hofu kwamba mlipuko mkubwa unaweza kuifanya iwe ngumu zaidi kwa vifaa muhimu kuingia nchini humo, na kusababisha uhaba wa chakula na uchumi unaodorora

Korea Kusini imesema ilitoa msaada wa kibinadamu baada ya tangazo hilo la Alhamisi, lakini Pyongyang bado haijajibu.

Licha ya madai ya hapo awali ya Korea Kaskazini kwamba ilikuwa na "mafanikio ya kung'aa" katika kuzuia Covid, kumekuwa na ishara wakati wote wa janga la uwepo wake nchini ikijumuisha ripoti ambazo hazijathibitishwa za kesi na wafanyakazi waliovaa suti za kujikinga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad