Wiki hii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee aliamua kutoa yake ya moyoni kuhusu marafiki zake kutomuunga mkono katika biashara zake.
JayDee alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao hawaungi mkoni biashara yake ya chakula, lakini wakishapiga ‘vyombo’ usiku wanaanza kumpigia simu mbele za watu ili waonekana wanamjua sana.
Anasema watu hao wakishapiga vyombo vyao wakasikiliza nyimbo zake basi wanaanza sifa za kujuana wakati hawaendi kumuungisha kwenye biashara zake na wala kwenye shoo zake hawaendi.
Siku moja baada ya kauli hiyo, mkongwe mwingine wa muziki wa Kenya, Nyota Ndogo aliyewahi kutamba na nyimbo za ‘Watu na Viatu’ na ‘Nibebe’ aliomshirikisha Nonini naye ametoa povu kuhusu mashabiki wanaokwenda hotelini kwake kula na kunywa bila kulipia huduma hiyo.
"Nasema sababu naona inazidi, tuko na Mashabiki na Marafiki.... watakwambia tunatafuta hoteli yako hatujui ilipo kisha wanakuja watano au sita wanaagiza kuku, pilau, nyama na kila kitu wakishamaliza kula wanakisifu chakula wanaingia kwenye gari wanaondoka zao.
"Mnakula chakula cha karibu 4000 Ksh. (Tsh. 79,000) mimi nina Watu nataka niwalipe nina kodi pia ya nyumba ya kulipa kama nyinyi ni Marafiki hamtokuja kula bure bali mtasema mnakuja kum-suport Nyota na huo sio Urafiki ni unafiki," - amesema Nyota.