Msichana wa miaka 13 anayedaiwa kubakwa na Wanaume wanne nchini India, anadaiwa kubakwa tena na Askari Polisi wakati alipokwenda kuomba msaada wa Polisi na kuripoti shambulio la kwanza.
Mamlaka ya Uttar Pradesh ilithibitisha kwamba Polisi huyo alikamatwa kutokana na kitendo chake hicho kilichozua taharuki nchini humo huku wengi wakiwashutumu polisi kwa kusaidia kuendeleza utamaduni wa ukatili wa kijinsia.
Wanaume wanne wamekamatwa kwa madai ya kumteka nyara na kumbaka mtoto huyo mwezi Aprili ambapo inadaiwa walimpeleka katika jimbo jirani la Madhya Pradesh ambako alibakwa na kuhifadhiwa kwa siku 4.
Ofisi ya Kitaifa ya rekodi za uhalifu nchini India inasema kuna zaidi ya kesi 28,000 za madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya Watoto nchini humo kwa mwaka 2020 pekee lakini Wanaharakati wanaamini kuwa idadi halisi ni kubwa zaidi.