Mapya yaibuka KIFO cha baba wa Nick minaj

 




Kumekuwa na taarifa tofauti kuhusu kifo cha baba mzazi wa mwanamuziki maarufu Nicki Minaj anayedaiwa kuuwawa na mwanaume mmoja aitwaye Charles Polevich na kwa mujibu wa TMZ, Polevich amekiri kuhusika na kifo cha Robert Maraj.


Ripoti zinaonyesha kuwa anashtakiwa kwa kosa moja la kuondoka eneo la tukio bila kuripoti na shtaka moja la kuharibu ushahidi wa mwili ambapo makosa yote mawili ni ya kihalifu.


Kwa mujibu wa ushahidi uliopatikana kutoka kwa mashuhuda na camera za barabarani CCTV Charles alimgonga na gari marehemu Robert na kukimbia kusikojulikana mnamo Februari 2021.


Katika ajali hiyo mbaya, inathibitka kuwa Charles alimgonga Robert kwa gari lake alipokuwa akivuka barabara huko Mineola, eneo la karibu na jiji la Long Island, New York nchini Marekani.


Kufuatia uchunguzi ulifanyika, mamlaka ilithibitisha kwamba Charles alitoka kwenye gari lake ili kuangalia kama Robert alikuwa sawa kabla ya kutoroka eneo la tukio bila kuwaarifu polisi au kumsaidia kwa namna yeyote baba wa mwimbaji huyo wa muziki wa rap.


Licha ya Charles kukabiliwa na makosa makubwa yaliyopelekea umauti wa baba wa mwanamuziki Nick Minaj, utata mpya unaibuliwa na hukumu ilitolewa na mahakama juu ya kesi hiyo, ambapo inadaiwa kuwa alihukumiwa mwaka mmoja jela, jambo ambalo halijauridhisha upande wa muathiriwa.


Indaiwa kuwa kaimu Jaji wa Mahakama Kuu ya Jimbo, Howard Sturim alimshauri Charles kuhusu masharti ya makubaliano ya rufaa, akisema, “Nitahukumu kifungo cha si zaidi ya mwaka mmoja jela.”


Charles hapo awali alikuwa anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 11 gerezani, na baada ya kuachiliwa, atahitajika kukamilisha huduma za kijamii, Pamoja na kufungiwa leseni yake, Mama mzazi wa Nicki, Carol Maraj, alizungumza kuhusu sentensi hiyo fupi.


“Sijafurahishwa na hilo, mwaka mmoja jela. Sijafurahishwa na hilo, nilikuwa na hasira sana, Nilianza kutetemeka kwa sababu ilirudisha kumbukumbu zote za usiku ule nilipokuwa nimekaa hospitalini,” alisema Carol mama wa Nick Minaj.


Ipo taarifa inayodokeza kuwa Charles anatarajiwa kurejea mahakamani ifikapo tarehe 3 Agosti licha ya kuwa bado haijafahamika ni hatua gani zaidi zitafuta kufuatia malalamiko ya upande wa familia ya Marehemu Robert Maraj.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad