Mjanja wangu nambari moja. Mshua flani poa sana aliyekuwa anapenda sana samaki.
Aliwahi kunichapa mara moja tu na vijiti vya mihogo pale kwetu kijitonyama sikuumia ila nililia kwa sababu hakuwahi kunichapa kabla.
Mzee Masoud ndiye aliyenipeleka kilimanjaro hotel, sio kula kuku, kununua rangi za maji za kuchorea. Nilipiga dili moja nikiwa na miaka 14 nikalipwa Tzs 2,500 nikamwambia naskia kuna duka pale kilimanjaro wanauza rangi. Akanichukua kwenye gari ya serikali (matumizi mazuri ya mali ya umma ) akanipeleka akaniacha nikanunua rangi nikaanza kurudi kwa miguu mpaka magomeni kwa bi mkubwa.
Nilipofika magomeni nikaanza kuchora nonstop mpaka leo hii.
Huyu mzee pamoja na mengine hakuwahi kunikataza kuchora.
Ameishi duniani kwa takriban miaka 93.
Kanifundisha mengi sana, kwa maneno na kwa vitendo zaidi.
Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa zawadi ya mzee wetu huyu aliyejaaliwa kuona mpaka vitukuu vyake.
Pamoja na kwamba ng'ombe hanenepi siku ya mnada lakini nisaidie kumuombea kwa Allah ampe kauli thabit na amfanyie wepesi kwenye utaratibu mpya aliouanza leo mpaka siku ya hukumu.
Msiba uko kijitonyama, tunazika leo saa kumi jioni in shaa Allah.