Kocha Msaidizi wa Namumgo na mchezaji wa zamani wa Simba Jamuhuri kiwelu Julio amesema, ni jambo jema kwa uongozi wa simba kuachana na nyota wao Bernard Morison kwani hakuwa na msaada wowote katika kuisaidi Simba icheze kama timu ndani ya uwanja zaidi uwezo wake binafsi.
Julio amesema uwezo huo ndio ulikuwa ukionekana kinyume kabisa na mahitaji soka la kileo, akiamini simba watampata Morrison mwingine kwani wamepita mastaa wengi kwenye klabu hiyo kumzidi.
Ameendelea kusema kuwa atashangazwa sana kama uongozi wa yanga wakiamua kumrejesha mchezaji huyo, ambaye aliwasumbua hapo kabla ili tu kuikomoa Simba.
Hata hivyo, taarifa kutoka Yanga, zinasema kuwa tayari mabosi wa timu hiyo wameshaanza kuangalia namna ya kumrudisha Morrison nyumbani, ambapo aliondoka misimu miwili iliyopita kwa uhamisho uliozua utata kwenye Soka la bongo, kiasi cha Yanga kufungua kesi CAS.
Inaelezwa kuwa endapo mamabo yataenda vyema, Morrison atapewa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongezwa endapo atakuwa kwnye kiwango bora huku suala la nidhamu yake likipewa pia kipaumbele.