Kampuni inayomiliki APP (program tumishi) ya WhatsApp yenye watumiaji zaidi ya bilioni mbili duniani kote, imesema inashughulikia kipengele kipya ambacho kitamuwezesha mtu ku-left; yaani kujitoa kwenye group lolote la Whatsapp kimyakimya bila wenzako kukushtukia huku ikisema kipengele hicho kinalenga kuwapa watumiaji uhuru.
Kwa sasa ni kawaida kwamba, mtumiaji yeyote wa WhatsApp anaweza kuona kama mtu mwingine ameungwa kwenye group, lakini pia anaweza kuona pale mtu anapojiondoa (anapo-left), lakini kwenye kipengele hiki kipya ni Admin pekee atakayeweza kuona kuondoka kwa mwanachama wake.
Hata hivyo, hadi sasa Kampuni ya Meta Platforms Inc yenye makao yake makuu nchini Marekani (zamani Facebook) ambayo ni kampuni mama ya WhatsApp haijaweka wazi tarehe ya kuzinduliwa kwa kipengele hicho.