Mtaka ataka matrafiki kukamata viongozi wa Serikali wanaokiuka sheria



Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (RC), Anthony Mtaka amewagiza matrafiki kuwakamata viongozi na madereva wa Serikali wote wanaokiuka sheria za usalama wa barabarani na kuwatoza faini.

Akizungunza leo Jumamosi Mei 19,2022  na askari polisi wa mkoa wa Dodoma, Mtaka amesema watakapowakamata na kupiga simu kwake atawaeleza lengo ni Mkoa wa Dodoma uwe salama.

“Tukilianza hivi leo tutatengeneza kizazi kinachoheshimu vitu, tukilimezea hivi tunakuja kutengeneza generation (kizazi ) ngumu kuna vitu ambavyo tunatakiwa kukataa kuvirithi, kuvunja sheria hakupaswi kurithiwa,”amesema.

Amesema hata yeye akiwa anaendesha gari yake binafsi na ikitokea amekamatwa amekuwa akilipa faini na hivyo hivyo kwa mkewe pamoja na dereva wake.


 
Mtaka amesema hata atakapopata simu zinazowaeleza kukukamatwa kwa viongozi atawaeleza kuwa walipe kwasababu wamekiuka sheria.

Amesema kwa kufanya hivyo kutawafanya wanaoingia ama wanaoishi Dodoma wataelewa kuwa ni mkoa wa kufuata sheria za usalama wa barabarani.

Mtaka amesema watu wamekuwa wakilalamika madereva wa Serikali na viongozi wamekuwa hawachukuliwi hatua za kisheria wanapovunja sheria za usalama wa barabarani jambo ambalo limewafanya kutukanwa.

“We kamata halafu waambie kuwa huu mkoa tumeshachoka kuripoti matukio ya ajali tunataka media ziliripoti matukio ya miradi ya maendeleo,”amesema.

Amesema wakiwakamata watu walili watatu watu watafuata sheria za usalama wa barabarani na kuwa salama.

“Ndio maana hamkamati watu wale ambao mnaowakamata wanageuza kwamba mnawaomba fedha. Kamata ili watu wajue kuwa mnamaanisha,”amesema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad