Rogers Kyaruzi raia wa Tanzania aliyeuawa nchini Marekani
MTANZANIA Rogers Kyaruzi mwenye umri wa miaka (30), aliyehamia Marekani akiwa mdogo, ametambulika kuwa ndiye aliyeuawa kwa kupigwa risasi na Polisi huko Atlanta, Georgia, Jumatano ya Mei 4, 2022 nchini humo.
Kyaruzi alikuwa milionea ambaye alimiliki tovuti maarufu ya flyheight.com na alikuwa akijihusisha na biashara za real estate nchini humo. Kyaruzi ambaye alikuwa mkazi wa Warner Robins, aliuawa akiwa na mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka mitano. GBI wanaendelea na uchunguzi.
“Nilishangaa, sikuamini,” alisema Myra Yorke, ambaye ni dada wa Kyaruzi wakati akihojiwa Alhamisi iliyopita na vyombo vya habari nchini humo.
“Sijui nini kilikuwa kinaendelea. Hatuna taarifa sahihi na za kutosha,bado tunasubiri ripoti ya uchunguzi. Askari aliyemuua bado hajaanikwa lakini wanasema alikuwa akifanya kazi ya ziada kwani hakuwa zamu, na alikuwa amevalia sare za polisi na camera ya mwilini wakati alipoitwa katika mgahawa wa Roasters Rotisserie uliopo Lenox Village,” alisem Yorke.
Polisi walifika eneo la tukio kwa ajili ya kuanza shughuli za uchunguzi
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa Mgahawa huo na polisi, Rodgers alikuwa akiwasumbua wateja, ndipo polisi mmoja aliyekuwa maeneo ya karibu aliitwa, akafika na kumsihi Rodgers aondoke, lakini alikataa kutii amri ya polisi.
Kwa mujibu wa GBI, Kyaruzi alikuwa “akionyesha tabia za jeuri huku akitaka kusababisha ajali, Kyaruzi alisababisha usumbufu katika eneo hilo na polisi alipomfuata na kumtaka ashuke kwenye gari alikaidi, wakati wa purukushani hizo kwa bahati mbaya risasi ilichomoka na kumpiga