Mtoto Adaiwa Kunyongwa na 'House Girl' Dar




Dar es Salaam. Mtoto Erickson Kimaro (8) pichani anadaiwa kunyongwa na dada wa kazi (jina halijajulikana) leo Me 31 jijini hapa.

Tukio hilo la kusikitisha linadaiwa kutokea majira yaa saa 11 jioni nyumbani kwao na mtoto huyo Kimara Temboni Jijini Dar es Salaam mara baada ya kurudi kutoka shuleni.

Mwanachi imepata habari hizo kutoka kwa majirani wa familia ya mtoto huyo baada ya kubaini mauaji hayo huku wakibahatika kushuhudia video iliyoonyesha tukio hilo.

"Ndani kulikuwa na CCTV Camera ndiyo imelionyesha tukio kabisa, kusema kweli sijawahi kuona mtu akinyongwa Ila nimeshuhudia inatisha sana kuweni makini sana na wadada," anasema jirani wa familia hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Mama Aika.


Mama Aika amesema mtoto huyo alikuwa mkarimu anasalimia watu akisoma shule ya Shule ya Anazack na mwanae.

Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake, baba mzazi wa mtoto huyo, Erick Kimaro amesema binti huyu wa kazi hakuwa na muda mrefu nyumbani hapo. "Huyu binti alikuja jumamosi na rafiki wa mke wangu ndiye aliyetutafutia kakaa tu jumapili na jumatatu na kufanya tukio hilo hatufahamu kabisa hata kwao," amesma baba wa mtoto huyo.

Naye mama mzazi wa mtoto huyo, Siriwa Kimaro amesema tukio hilo limetokea mara baada ya mtoto huyo kurudi kutoka shuleni


Siriwa amesema baada ya binti huyo kufanya tukio hilo alimpigia simu kumwambia mtoto ana hali mbaya na ndipo alipotoka kazini na kuwahi kurudi nyumbani.

"Nafika tu namkuta mwanangu amelala ubavu mdomo na macho yako wazi uso umejaa na shingoni pamevijia damu kumshika shingoni kawa wa baridi ila mdomo uko wazi kama alikuwa akitafuta hewa," anasema mama mzazi wa mtoto huyo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema taarifa hizo wamezipata kutoka kwa wazazi wa mtoto huyo.

"Tunamuhoji huyo binti kwa uchunguzi zaidi kwa kifupi tunachunguza taarifa hiyo ambayo imeletwa na wazazi," amesema Muliro alipozungumza na kituo cha televisheni cha ITV.


Mwananchi imefika nyumbani kwa mama mzazi wa mtoto huyo na kukuta waombolezaji wakiwa na sura za simanzi na taratibu za mazishi zikiendelea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad