Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji amesema wastani wa bei ya rejareja ya cement kwa mfuko wa kilo 50 ni Shilingi 18,283, sawa na ongezeko la bei kwa asilimia 3.5 ukilinganisha na wastani wa bei ya Shilingi 17,662 ya mwezi Machi, 2021"
"Kwa ujumla wake bei za vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati na nondo zimeendelea kuwa juu kutokana na kuongezeka kwa bei za malighafi za vifaa vya ujenzi katika soko la dunia"
"Tathmini iliyofanyika ilibaini kuwa upandaji wa bei ya cement unatokana na uhaba unaosababishwa na mahitaji makubwa ya cement katika miradi ya kitaifa, usambazaji hafifu wa bidhaa hiyo kuwafikia watumiaji wa mwisho na ucheleweshaji wa upatikanaji wa saruji kutoka kiwandani"
"Wizara imeendelea kukusanya taarifa za bidhaa sokoni ikiwa ni pamoja na bei za mazao makuu ya chakula na mafuta ya kula katika masoko mbalimbali hapa nchini ili kuwafahamisha wananchi na wadau wengine kuhusu mwenendo wa bei za bidhaa mbalimbali"