Mwakalebela aishutumu Simba SC Ligi Kuu



Bao la pili la Simba SC dhidi ya Kagera Sugar lililofungwa na Mshambuliaji na Nahodha John Raphael Bocco jana Jumatano (Mei 11), limepingwa na Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Fredick Mwakalebela.

Simba SC iliichapa Kagera Sugar mabao 2-0, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, uliounguruma Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, matokeo yaliyochukuliwa kama kulipa kisasi kwa Mnyama kupoteza mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza kwa kufungwa 1-0, Uwanja wa Kaitaba.

Mwakalebela amesema bao la Bocco halikustahili kukubaliwa, kwa sababu kabla ya kufunga alikua ameotea, lakini cha kushangaza Mwamuzi msaidizi Frank Komba hakumsaidia vyema Mwamuzi wa kati Ramadhan Kayoko kwa kuonyesha kibendera kwa kuashiria kulikua na kosa limefanyika.

“Nimeliona lile bao lao la pili la Offside, wachezaji wawili wako ndani kabisa kwenye 18, wameshaingia dani kabisa, sasa kama mchambuzi hukuliona lile, unanisikitisha,”


 
“Hata lile la juzi dhidi ya Ruvu Shooting, uliona bao la Bocco, yaani kipa amefurahia kabisa kufungwa, na huko nyumbani kwake ninafikiria alifanya Pati,”

“Namaanisha Simba SC sio mpinzani wa kweli, Simba SC ana CHUPLI CHUPLI nyinyi tu, kwa nini asiifunge Young Africans, kwa nini haifungi Young Africans? Kwa ujanja ujanja tu, kwa nini hatufungi?”

“Hata ubingwa waliochukua unadhani walichukuwaje, watanzania wanaelewa kila kitu, hadi mimi nilifungiwa, unadhani mimi kwa nini nilifungiwa? Nililalamika kwa kufunya uchunguzi wa mechi zao zinakua hivi, na zetu nilikua hivi.”


“Msimu uliopita nilifanya uchunguzi walikua na Penati ngapi, Kadi Nyekundu ngani, Extra Time ngapi, Droo ngapi, na msimu huu mambo ni yale yale, mtu huwezi kumuongezea dakika hadi 107, kwa kitu gani kilichofanyika pale uwanjani?”

“Yaani Simba akiwa bila bila lazima afunge goli, yaani kwenye EXtra Time lazima afunge goli.” amesema Mwakalebela

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad