Mwanafunzi mzungu nchini Afrika Kusini amesimamishwa kimasomo kwa muda kutoka chuo kikuu baada ya kushutumiwa kwa kukojolea mali za mwanafunzi mweusi katika chuo kikuu cha Stellenbosch University, taasisi imeithibitishia BBC News.
Chuo kikuu kimesema kuwa tukio hilo litachunguzwa na kuchukua hatua ikiwemo kumfukuza na mashitaka ya uhalifu yanaweza kufunguliwa, itategemea na matokeo ya uchunguzi.
Wanafunzi kadhaa wameandamana katika Chuo kikuu cha Stellenbosch University Jumatatu wakidai hatua kali ilichukuliwe dhidi ya mwanafunzi huyo wa mwaka wa kwanza.
Chuo kikuu-sawa na mitandao ya kijamii ambayo imekuwa ikisambaza video -wamesema kuwa tukio hilo linaonekana kuwa lilichochewa na itikadi za ubaguzi wa rangi.
Katika taarifa yake, msemaji wa kikuu cha Stellenbosch Martin Viljoena amesema kuwa chuo kikuu "kinalaani vikali tukio la uvurugaji, usikitishani na ubaguzi”.
Muathifriwa bado ameshangaa na anajaribu kufikiria kilichomtokea, chou kikuu kimesema.
Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, muathiriwa alikuwa amesinzia wakati alipoamka aliposikia mtu akiingia chumbani kwake.
Katika video hiyo anasikika akimuuliza mwanafunzi mzungu ni kwanini alikuwa anakojolea mali zake.
Tukio hilo kwa mara nyingine tena limeangazia makabiliano dhidi ya ubaguzi wa rangi uliosheheni nchini humo miongo kadhaa baada ya kuisha kwa ubaguzi wa rangi.