Ndege ndogo ya abiria iliyokuwa imebeba watu 11 imenguka katika msitu karibu na mji mkuu wa Cameroon, Yaoundé, siku ya Jumatano, wizara ya uchukuzi imesema.
Sababu ya ajali hiyo haikufahamika mara moja, lakini ndege hiyo ilipoteza mawasiliano ya redio na waongozaji wa ndege na baadaye ilipatikana katika msitu karibu na Nanga Eboko, karibu kilomita 150 (maili 90) kaskazini-mashariki mwa Yaoundé, wizara ilisema katika taarifa.
Ndege hiyo ilikuwa ikiruka kutoka uwanja wa ndege wa Yaoundé Nsimalen kuelekea Belabo, mashariki mwa nchi, iliongeza.
Shirika la habari la AFP linanukuu vyanzo rasmi vikisema ndege hiyo ilikodiwa na kampuni binafsi ya Usafirishaji wa Mafuta ya Kameroon (COTCO) yenye bomba la hydrocarbon linalopita kati ya Cameroon na nchi jirani ya Chad.
Inasema ajali hiyo ilikuwa janga kubwa la kwanza la anga kuwahi kutokea nchini tangu 2007, wakati ndege ya shirika la ndege la Kenya Airways iliyokuwa na watu 114 kuanguka baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Douala.
Msako wa kuwatafuta manusura unaendelea.