Polisi Arusha Wateketeza Ekari 4 za Bangi

 


Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kuteteketeza Ekari Nne na nusu za Bhangi, katika  maeneo ya kisimiri juu, kitongoji cha Luwai na Jangwale Katika Halmashauri ya wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.



Mkuu wa Oeresheni za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msaaidizi wa Polisi ACP Gaudianus Kamugisha amesema kuwa tarehe 21.05.2022 muda wa saa 11:00 alfajiri, huko maeneo ya huko maeneo ya kisimiri juu, kitongoji cha Luwai na Jangwale Katika Halmashauri ya wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.Jeshi la Polisi lilifanikiwa kuteketeza bhangi ekari nne na nusu pamoja na Bhangi yote iliyokuwa shambani na nyumbani ambayo ni kiasi cha gunia 10 pamoja na debe moja la mbegu ya Bhangi kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya vijiji, 


Ameendelea kusema operesheni hiyo ni mwendelezo wa operesheni zinazofanyika mara kwa mara katika mkoa wetu kwa ajili ya kupambana na kilimo cha bhangi pamoja na watumiaji wa madawa hayo.


ACP kamugisha amesema kuwa watuhumiwa wanaoishi katika nyumba hizo (maboma) yalikopatikana magunia ya Bhangi hizo walikuwa tayari wameshakimbia katika nyumba zao. Hivyo alisema Jeshi la polisi mkoani humo linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa hao.

ACP Kamugisha ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi lao kwa kutoa taarifa ya watu wanaojihusisha na kilimo cha Bhangi katika maeneo yao, pia natoa wito kwa baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya kuacha mara moja, kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad