Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba mahesabu ya nyongeza ya kima cha mshahara yanaendelea na kukataa kile kiwango cha milioni 1 na elfu 10 kilichotajwa na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA).
Kauli hiyo ameitoa hii leo Mei Mosi, 2022, wakati akizungumza na wafanyakazi pamoja na wananchi walijitokeza mkoani Dodoma wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi dunia inayojulikana kama #MeiMosiDay
"Ulezi wa Mama unaendelea, yale mambo mbalimbali tuliyoyafanya mwaka huu kupunguza kodi hiki na kile tutaendelea kuyafanya, jambo letu lipo (Mshahara) si kwa kiwango kilichosemwa na TUCTA kwa sababu mnajua hali ya uchumi wa nchi yetu na Dunia hali si nzuri sana, nimeagiza jambo liwepo, mahesabu yanaendelea, tutajua lipo kwa kiasi gani," amesema Rais Samia