Rais Samia akanusha taarifa kwamba alikuwa haelewani na Magufuli



RAIS Samia amesema alinukuliwa vibaya na vyombo vya Habari vilivyosema kwamba alisema hakuwa na maelewano mazuri na Rais John Magufuli kipindi yeye akiwa Makamu wa Rais. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rais ametoa ufafanuzi huo katika mahojiano na kituo cha UTV yaliyorushwa leo Jumatano tarehe 4 Mei 2022 baada ya kuhojiwa na Mkurugenzi mwendeshaji wa Azam Media, Todi Mhando kuhusu ukweli wa taarifa hiyo.

“Kama walinikuu hivyo basi walikosea, unakuaje makamu wa rais halafu usiwe karibu na rais na hilo ndiyo swali limeshajijibu hivyo,”

Mbali na hayo Rais Samia amesema amejifunza kutoka kwa Rais John Magufuli kusimamia nidhamu ya kazi “lakini pili kuwe na tija katika kufanya kazi na ndiyo maana marehemu (Rais Magufuli) alikuwa mkali sana kutaka kuona matokeo ya kinachofanywa kwahiyo kile na mimi kilinipa mafunzo sana.”


 
Amesema ukali unaweza kuwa wa maneno na unaweza kuwa wa matendo na kukiri kuwa yeye hana ukali wa maneno, “lakini kwa matendo mtu unaweza kufanya kitu mtu anakuelewa mama amekusudia kuzungumza kitu.”

Vilevile amezungumzia miradi iliyoachwa na mtangulizi wake na kufafanua kuwa hiyo ni miradi yao na si ya Rais Magufuli kwani naye alikuwepo katika Serikali iliyoianzisha.


John Magufuli, Mgombea Urais na Mgombea mwenza wake, Samia Suluhu wakirudisha fomu za kugombea urais
Rais Samia amesema miradi yote waliyoanzisha awamu ya tano ina maana kubwa kwenye wimbi la nne la mapinduzi ya viwanda, “tunapozungumza biashara huru ndani ya Afrika maana yake ni kuwa na njia za usafiri, muwe na reli, muwe na bandari, muwe na barabara na muwe na umeme wa kutosha hata kuuza kwa wengine.”


Alisema changamoto kubwa ni ukubwa wa miradi na uwezo wa ndani wa nchi “ile miradi tulikuwa tunaiendesha kwa mikopo na kwa wakati ule mikopo ambayo tulikuwa tunaipata na hali ya maradhi na kwamba mashirika ya kimataifa ya fedha yalishatengeneza mipango yake kwamba kwa Tanzania tutaoa pesa mwaka huu hizi na hizi kwahiyo miradi haikupata nafasi kwa mwaka ule.”

Alifafanua zaidi kuwa ni sahihi kusema tumejenga kwa fedha zetu kwasababu ni mikopo ambayo itarudishwa kwa wakopeshaji.
“Kama nakuambia nikopeshe nitakulipa ile pesa ni yangu kwasababu nitakulipa kwahiyo tulijenga kwa pesa zetu lakini kwa kukopa. Kwahiyo tatizo ni itaendeleaje lakini nashukuru Mungu.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad