Rais Samia Ataja Waliochangia Filamu ya Royal Tour

 


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka wazi mchakato wa kufanya filamu ya Royal Tour ikiwa ni pamoja na jinsi fedha za kufanya filamu hiyo zilivyochangwa na watanzania mbalimbali.

Rais Samia akizungumza katika uzinduzi wa filamu hiyo leo Mei 8/2022 Jijini Dar es salaam ameweka wazi kuwa fedha zilizotumika kuilipa kampuni iliyofanya filamu hiyo ni Bilion 7 .

"Tarehe 26 June mwaka jana 2021 Nilifanya kikao cha 12 cha baraza la biashara Tanzania na niliomba wana baraza waniunge mkono katika mradi huu, na tarehe 23 Augost huo huo mwaka jana nilifanya chakula cha hisani usiku na kuita wale wote walioahidi kuniunga mkono waje kuchangia, na michango ilikwenda vizuri" amesema Rais Samia.

Aidha amesema lengo lilikuwa kukusanya bilioni 20 lakini kwa uwezo wa Mungu alipata ahadi za bilioni 19 na milioni 39, ambapo pia jumla ya makusanyo ilikuwa ni bilioni 12 na milioni 759 

Amezitaja sekta zilizochangia kuwa ni Uwekezaji uzalishaji na biashara, sekta ya fedha na sekta ya utalii wote kupitia mabaraza yao

Rais Samia amesema kuwa fedha yote iliyokusanywa ndio iliyotumika kwenye Royal Tour huku bilioni saba zikitumika kulipa kampuni iliyoshot filamu hiyo

"Kulikuwa kuna hoja kadhaa kuhusu matumizi ya fedha, nataka nikiri kwenu kwamba fedha yote tuliyokusanya ndio iliyotumika kwenye Royal Tour, na tulitumia Bilioni 7 kulipa kampuni iliyofanya shooting na kutengeneza filamu nyingine" - amesema Rais Samia

Pamoja na hayo Rais Samia ameahidi ujio wa phase ya pili na ya tatu ya filamu hiyo ili kuendelea kuitangaa Tanzania

"Nataka niwaahakikishie bado tuna backup, kwa sababu Royal Tour phase one ndio hii tunaiona lakini walichukua picha nyingi sana ndani ya Tanzania, kwahiyo bado tutakwenda na phase two na phase three, kwahiyo fedha hii tuliyonayo tunakwenda kudevelop phase two na three ya Royal Tour" amesisitiza Rais Samia

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad