Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza waajiri kuaandaa malipo ya wastaafu wanaotarajia kustaafu kabla ya mtumishi kuondoka ofsini.
Amesema hakuna sababu ya watumishi kuendelea na usumbufu wa kusubiri mtandao kwa kuwa taarifa za mtumishi zinajulikana kwa mwajiri miezi sita kabla ya mfanyakazi kustaafu.
“Naagiza ndani ya kipindi cha miezi sita, maafisa raslimali watu wanapaswa kushughulikia taarifa za mtumishi. Mifuko nayo ifanye uhakiki wa malipo ya mfanyakazi kuepusha mizunguko,” amesema Rais Samia
Mwaka jana serikali ilitenga jumla ya Sh trilioni 2.17 kwa ajili ya kulipa deni la mafao kwa wanachama waliorithiwa kutoka uliokuwa mfuko wa pensheni wa PSPF na LAPF.
Kujenga mfumo wa kielektroniki uliounganishwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa NIDA, Malipo ya mafao yameanza kufanyika ndani ya siku 60.