Nchini Afrika Kusini, Rais Cyril Ramaphosa alilazimika kuondoka kwenye maadhimisho hayo baada ya wafanyakazi kumvamia kwenye jukwaa akihutubu.
Huku wakiimba Wakiimba "Cyril must go, Cyril lazima aondoke," waliinua mabango wakidai nyongeza ya mishahara wakati wa sherehe hizo zilizoandaliwa mjini Rustenburg.
Katika video ya dakika mbili ya tukio hilo, Rais huyo anaonekana akijaribu kuwatuliza wafanyakazi hao ambao walimzomea.
Wafanyakazi hao wa mgodi wa ndani ambao wamekuwa katika mgomo kwa wiki kadhaa, wanataka nyongeza ya mishahara ya kila mwaka ya rand 1,000 (KSh 7,173).
Magazeti Jumanne, Mei 3: Wakenya 6 Wafika Kortini Kuwazuia Raila, Ruto Kuwania Urais
Akijaribu kuzungumzia moja kwa moja suala hilo, Rais Ramaphosa alizomewa vikali na wafanyakazi hao.
Rais Uhuru Aamuru Nyongeza ya 12% kwa Wafanyakazi wa Chini
Kwingineko humu nchini, Rais Uhuru Kenyatta ameamuru nyongeza ya asilimia 12 kwa wanaopata mshahara wa chini maarufu kama minimum wage.
Kenyatta alisema kupanda kwa gharama ya maisha kunashawishi mshahara wa chini kuongezwa ili wafanyakazi waweze kujikimu wakati huu.
"Kwa sababu hatujaongeza mshahara wa chini kwa miaka mitatu iliyopita. Na kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, na tukiangalia wajibu wa wafanya kazi humu nchini, naamuru nyongeza ya asilimia 12 kwa mshahara wa chini itakayotekelezwa kuanzia hii leo," alisema Kenyatta.
Akihutuibu wakati wa sherehe za Leba Dei zilizofanyika katika uwanja wa Nyayo Jumapili Mei 1, Rais alilaumu Covid-19 na vita vinavyoendelea katika ya Urusi-Ukraini katika kuathiri gharama ya maisha.
Tangazo la Rais Kenyatta linamaanisha kuwa Mkenya anayepokea mapato ya chini zaidi sasa ataweka mfukoni Ksh20,680 kutoka Ksh17,240.
Wetang'ula amtaka Uhuru Apunguze Hasira "Utaruka Akili Bure"
Katibu Mkuu wa Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli hapo awali alikuwa ameshawishi kuongezwa kwa asilimia 40.
Hata hivyo, baada ya mazungumzo na Shirikisho la Waajiri wa Kenya - FKE, waliweza kushuka hadi asilimia 23, takwimu ambayo Rais alitmiza nusu yake tu.