Real Madrid imetinga fainali ya Uefa baada ya kuifunga Manchester City jumla ya mbao 6-5
KLABU ya Real Madrid imefanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya maarufu kama UEFA baada ya kuitandika klabu ya Manchester City kwa jumla ya mabao 3-1.
Real Madrid imeitoa Manchester City kwa tofauti ya mabao 6-5 kwani kwenye mchezo wa awali Manchester City ilishinda bao 4-3 kabla ya Madrid kupindua kibao na kushinda kwa mabao 3-1.
Iliwachukua Man City dakika 73 kuandika bao lake la kwanza kupitia kwa Riyad Mahrez kabla ya Rodrygo kusawazisha na kuongeza kunako dakika ya 90 na 91.
Mshambuliaji hatari Karim Benzema aliongeza bao la 3 katika dakika ya 95 kupitia mkwaju wa penati na hivyo kukatisha ndoto za Manchester City kushiriki Fainali ya pili mfululizo ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.
Vurugu zilitokea wakati wa mchezo huo ambao ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-1
Kwa matokeo hayo Real Madrid itaungana na Liverpool kushiriki Fainali ya Kombe la Uefa huku Liverpool ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza fainali hiyo kwa mabingwa hao mara 13 mara baada ya kukutana Mei 26 2018 ambapo Liverpool iliambulia kichapo cha mabao 3-1.
Fainali ya Ligi ya Mabingwa inatarajiwa kufanyika Mei 29 mwaka huu katika Jiji la Paris nchini Ufaransa.