Salah na Son wagawana Kiatu cha Dhahabu baada ya kuibuka wafungaji bora wa EPL msimu huu





FOWADI Mohamed Salah wa Liverpool na Son Heung-min wa Tottenham Hotspur waligawa tuzo ya ‘Kiatu cha Dhahabu’ baada ya kila mmoja wao kupachika wavuni mabao 23.

Son alifuma wavuni mabao mawili katika ushindi wa 5-0 waliosajili dhidi ya Norwich City naye Salah akafunga goli moja dhidi ya Wolves.

Ni mara ya tatu kwa Salah kuibuka Mfungaji Bora wa EPL. Alitwaa kiatu cha dhahabu mnamo 2017-18 baada ya kufunga mabao 32 na 2018-19 alipokamilisha msimu kwa magoli 22 sawa na mwenzake wa Liverpool, Sadio Mane, na aliyekuwa fowadi wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang.

Kati ya mabao ya Salah msimu huu ligini, 20 yalifumwa kimiani kabla ya Machi 12 na matatu yakafungwa katika mechi moja (hat-trick) katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Man-United mnamo Oktoba 24, 2021. Raia huyo wa Misri alijishindia pia tuzo mpya iliyoanzishwa 2017-18 ya mchezaji aliyechangia mabao mengi zaidi ligini muhula huu (13).


 
Kwa upande wake, Son alipachika wavuni mabao tisa kutokana na mechi 10 zilizopita, yakiwemo sita katika michuano mitano ya mwisho wa muhula. Nyota huyo raia wa Korea Kusini naye alifunga hat-trick moja katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Aston Villa ugenini mnamo Aprili.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad