Mchambuzi wa Soka Saleh Ally maarufu kama ‘Jembe’ anadai Bernard Morrison muda wowote ule anaondoka nchini kwenda kwao Ghana
MCHAMBUZI wa soka kutoka kipindi cha Krosi Dongo kinachorushwa na 255globalradio na Global TV ametoa habari za ndani kabisa kuhusu mustakabali mzima wa mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Ghana Bernard Morrison na hatima yake ndani ya kikosi hicho chenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, Kariakoo Jijini Dar es Salaam.
Saleh Ally Maarufu kama ‘Jembe’ anadai alipata fursa ya kuongea na Bernard Morrison na moja ya kitu alichomhakikishia ni kwamba amechukua mizigo yake na tayari anaondoka kuelekea kwao Ghana kwani anaona kabisa kama haitajiki tena na klabu ya Simba.
Saleh Ally ‘Jembe’ akiwa ndani ya Studio za 255globalradio na Global TV
Jembe anadai kwa maelezo ya mchezaji huyo kikwazo kikubwa na Mtendaji mkuu wa Klabu hiyo Barbara Gonzalez ambaye anadaiwa ndiye aliyetoa maelekezo ya Morrison kuondolewa katika kikosi cha wachezaji wa Simba, na ile hojaya kwamba Morrison ana matatizo ya kifamilia si ya kweli kwani Morrison mwenyewe amethibitisha kuwa hana matatizo yoyote yake ya kifamilia.
Kwa mujibu wa Bernard Morrison anadai kuwa amefanya jitihada nyingi za kuhakikisha kuwa anasaini mkataba mpya ikiwemo uwabembeleza baadhi ya viongozi ili abaki msimbazi lakini Mtendaji Mkuu Barbara amekuwa mwiba mkali wa kuzui hilo lisitokee na badala yake wakati mazungumzo yakiwa yanaendelea akapewa likizo ya lazima.
“Ameniambia mi naenda kutoa vitu vyangu vyote kwenye nyumba ya Simba kesho naondoka naenda nyumbani kama ntapata muda tutafanya Interview lakini kama nikikosa nikirudi tutafanya interview.”alinukuliwa Saleh Jembe akiongea kuhusu Morrison.
Bernard Morrison alitolewa kwenye kikosi cha Simba kinachoendelea kushiriki mashindano ya Ligi Kuu ya NBC kwa sababu ya kuwa ni ana matatizo ya kifamilia jambo linalomfanya kuwa nje ya uwanja hadi mwisho wa msimu huu.