Mfumo wa mchezaji kutumia robo tatu ya maisha yake kambini sidhani kama upo sawa, naamini Professional ana mkataba wake ambao anapaswa kuhukumiwa kwa matokeo uwanjani, lazima tuwe results oriented
Wachezaji ni binadamu kama walivyo Viongozi wa hizi timu, wana mahitaji ya kibinadamu ambayo ni kawaida, ni lazima kuwe na flexibility ili kukidhi matakwa ya kibinadamu
Sipingani na kanuni za klabu ila modern football lazima tubadilike, uhuru uwepo lakini wenye kukidhi matokeo, ambayo naona kwa anayejitambua atakupa tu matokeo