Mtawala alieshikilia mamlaka ya Umoja wa Falme za Kirabu kwa muda mrefu Sheikh Mohamed bin Zayed Al-Nahyan, amechaguliwa kuwa rais wa taifa hilo leo, siku moja baada ya kifo cha kiongozi wa zamani Sheikh Khalifa.
Shirika la habari la UAE limesema Sheikh Mohamed amechaguliwa na Baraza Kuu la Shirikisho, na kuwa mtawala rasmi wa taifa hilo lenye utajiri wa mafuta lililoasisiwa na baba yake mnamo 1971.
Sheikh Mohamed alikutana na Baraza Kuu la Shirikisho, linaloundwa na watawala wa imaarat saba za UAE, wakati taifa hilo likiingia kipindi cha maombolezo ya kifo cha kaka yake Sheikh Khalifa.
Kutawazwa kwake ambako kulikuwa kunatarajiwa pakubwa, kunarasimisha nafasi yake kama kiongozi wa taifa hilo la jangwa lenye wakaazi milioni 10, baada ya miaka kadhaa ya kuongozea nyuma ya pazia kutokana na ugonjwa wa kaka yake