Simba Washindwa Kufurukuta Mbele ya Azama, Yanga Sasa Njia Nyeupe Ubingwa




KLABU za Simba na Azam FC zimetoshana nguvu kwa sare ya mabao 1-1, kwenye mchezo wa mzunguko wa 24 wa Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi, majira ya saa 1 usiku nakushuhudia Simba ikidondosha alama mbili muhimu katika harakati za kuwania ubingwa.

Kwenye mchezo huo Azam FC ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Rogders Kola dakika ya 37, kabla ya dakika saba baadae Nahodha wa Simba, John Raphael Bocco kuisawazishia bao hilo na kufanya mchezo huo kwenda mapumziko ya sare ya bao 1-1.

Kipindi cha pili kiliporejea timu hizo zilishambuliana kwa zamu katika nyakati tofauti, lakini hakuna iliyofanikiwa kuona lango la mwenzake kwa mara ya pili.




Kwa matokeo hayo Simba inaendelea kusalia kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 50, ikiwa ni tofauti ya pointi 10 nyuma ya Yanga ambao ni vinara wa Ligi hiyo wakiwa na pointi 60.

Kwa sasa Yanga wanahitaji alama tisa sawa na michezo mitatu, ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa mara ya 28.

Mara baada ya mchezo huo kikosi cha Simba kitasafiri kuelekea mkoani Geita, ambapo siku ya Jumapili tarehe 22 Mei 2022, watashuka dimbani majira ya saa 10 jioni kuikabili Geita Gold.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad