Simba yawatoa Hofu Mashabiki Uwepo wa Chama na Kapombe



WAKATI mashabiki wa Simba wakiwa na hofu ya kukosekana kwa baadhi ya mastaa wa kikosi cha kwanza, uongozi wa klabu hiyo imewatoa wasiwasi na kueleza maendeleo ya nyota hao huku ikiamini watakuwa sehemu ya mchezo huo.

Baadhi ya wachezaji ambao wanauguza majeraha ni Aishi Manula na Shomari Kapombe walioumia Jumapili iliyopita katika mchezo wa ligi dhidi ya Geita Gold ambapo Manula aliangukiwa na kioo akaumia vidole huku Kapombe akichanika nyama za paja.

Wengine ni Clatous Chama, Chris Mugalu na Jonas Mkude waliokuwa na majeraha ya muda mrefu.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza, Meneja Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema wachezaji Kapombe, Manula na Chama wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri huku wakiwa na matumaini kuwa hadi kufika Jumamosi watakuwa sehemu ya kikosi.


Amesema Chama alianza mazoezi binafsi jumatatu na jana amefanya mazoezi na wenzake huku Chris Mugalu akirejea kikosi lakini mchezaji pekee watakayemkosa ni Jonas Mkude ambaye aliachwa jijini Dar es Salaam.

"Wachezaji wetu majeruhi Manula na Kapombe wanaendelea na matibabu tunaamini hadi siku ya mchezo watakuwa tayari, Chama alikuwa majeruhi lakini Jumatatu alifanya mazoezi binafsi kwa namna ambavyo anaimprove anatia matumaini,"

"Mugalu yuko sawa alishaanza mazoezi na wenzake kabla ya mchezo na Geita, kwasasa tutamkosa Mkude ambaye ni majeruhi tulimuacha Dar es Salaam anaendelea na matibabu," amesema Ahmed.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad