Spika wa Bunge Dk Tulia Ackson.
SPIKA wa Bunge Dk Tulia Ackson ametaka serikali kuwaelekeza madereva wa viongozi wakiwemo mawaziri kuzima magari na kushuka mara baada ya viongozi kufika katika maeneo husika na kushuka kwenye magari hayo.
Dk Tulia alitoa ombi hilo mara baada ya kipindi cha maswali na majibu bungeni ambapo alidai madereva wa viongozi bado walikuwa wakiendelea kubaki kwenye magari huku yakiwa yana unguruma ijapokuwa viongozi wako bungeni.
“Katika juhudi zinazo fanywa na serikali za kubana matumizi, liko jambo nimekumbushwa mapema leo. Magari ya viongozi ikiwa ni pamoja ya mawaziri na naibu mawaziri yanaendelea kuwaka hapo nje wakati sisi tuko humu ndani.
“Waheshimiwa wabunge mjue, lakini pia upande wa serikali tunatamani magari ya viongozi yakisha mshusha kiongozi bungeni ama nchi nzima ikishamshusha awe ni katibu mkuu awe meya au kiongozi wowote ikiacha viongozi ambao kwa itifaki yao magari yao yanapaswa kuendelea kuwaka ni matumizi mabaya ya fedha za serikali,” amesema Spika Tulia