Sweden na Finland zawasilisha Rasmi Maombi ya Kujiunga NATO

 


Mabalozi wa Sweden na Finland wamewasilisha rasmi maombi yao ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO leo kwa Katibu Mkuu Jens Stoltenberg. 

Hayo yamefanyika katika hafla ya video mjini Brussels. Akiyakubali maombi hayo, Stoltenberg amesema hatua hiyo ni ya kihistoria katika wakati muhimu sana kwa usalama wa Ulaya.


"Wanachama wa NATO sasa watazingatia hatua zinazofuata kuelekea nchi zenu kuwa wanachama. Usalama wa wanachama wote lazima uzingatiwe pia katika mchakato huu na tunadhamiria kuangazia masuala yote na tupate suluhisho la haraka."


Urusi imesema maombi hayo ya Sweden na Finland kutaka kuwa wanachama wa NATO hayaleti tofauti yoyote kwa kuwa nchi hizo zimekuwa zikishiriki luteka za kijeshi na muungano huo wa kujihami.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad