Taliban Yatoa Amri Wanawake wote wa Afghanistan Kuvaa Nikabu Uraiani



Aina ya vazi linalotakiwa kuvaliwa na mwanamke wa Afghanistan anapotoka nje ya makazi yake

SERIKALI ya Taliban imepiga marufuku kwa wanawake nchini humo kutembea bila kuvaa Nikabu (Nguo maalumu ya kuficha uso) katika maeneo ya wazi au uraiani.

 

Waziri wa muda wa maadili, Khalid Hanafi amesema:

 

“Tunataka dada zetu waishi kwa maadili yenye hadhi na usalama.”

 

Nikabu ya bluu imekuwa alama duniani kote ya mwanamke wa Afghanistan tangu miaka ya 1996 hadi 2001 na maamuzi ya kulifanya vazi hilo kuwa la lazima kuvaliwa yanazidi kuashiria ongezeko la vikwazo wanavyokumbana navyo wanawake kuonekana sehemu za wazi.

 

Amri hiyo inasema kuwa mwanamke ambaye hataficha uso wake kwa nikabu nje ya nyumbani, baba yake au nduguyake wa karibu wa kiume atatembelewa na atafungwa jela au kama ni mtumishi wa umma atafukuzwa kazi.

 

Lakini pia amri hiyo inaeleza kuwa kama mwanamke hana shughuli inayomlazimu kukaa nje ya nyumbani kwake kama vile biashara basi ni bora tu abaki nyumbani kwake.

“Misingi ya kiislam na dhana za kiislam ni muhimu sana kwetu kuliko kitu kingine chochote.” Alisema Hanafi.


Aina ya vazi linalotakiwa kuvaliwa na mwanamke wa Afghanistan kwa mujibu wa amri za Taliban

Wanawake wengi Afghanistan wanavaa mitandio kwa ajili ya ibada na shughuli za kidini lakini katika maeneo ya mjini hasa Kabul wanawake hawafuniki nyuso zao.

 

Jumuiya ya Kimataifa imeshauri Taliban waliangalie upya suala hilo

Kuelekea kulitawala tena Taifa la Afghanistan mwaka 2021 ambapo ilipiga marufuku Elimu na Ajira kwa wanawake. mara ya mwisho Taliban ilitawala Taifa la Afghanistan kuanzia mwaka 1996 hadi marekani ilivyoingilia kati mwaka 2001

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad