Utafiti uliofanywa mwaka 2017/2018 na kurudiwa 2021/22 katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Iringa, Mbeya na Mwanza imebainisha kuwa takribani watoto 7,778 wanaishi kwa kutegemea kazi za mitaani ikiwemo kuomba.
Takwimu zinasema kwa mwaka 2021/22 watoto hao walipungua kwa asilimia 27 ambacho ni kipindi cha miaka mitatu lakini tatizo bado ni kubwa na linawaathiri zaidi wavulana kwa kuwa wao hutumika zaidi kama nguvukazi katika maeneo ya mijini.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dkt. Dorothy Gwajima ametoa Takwimu hizo wakati akifungua mkutano wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Wanawake na Watoto MTAKUWWA leo Mei 25 jijini Dar es Salaam.
Dkt. Gwajima amesema kuwa watoto hawa hulala mitaani, katika vituo vya mabasi, nje ya maduka, pembezoni mwa Barabara, na wengine katika kingo za Bahari na Ziwa,
“Utafiti uliofanyika 202/22 ulionesha kuwa bado Dar es Salaam inaongoza kuwa na idadi kubwa ya wanaishi na kufanya kazi mitaani kwa asilimia 20 ikifuatiwa na mkoa wa Dodoma. Wengi wa Watoto hawa wamekuwa wakisafiri kutoka mikoa mbalimbali na kuhamia maeneo ya mijini. Na Njia kuu wanazotumia kufika mijani ni kujificha chini ya uvungu wa Malori. Hapa tunatengeneza vikosi vya hatari sisi wenyewe,” Dkt Gwajima amesema.
Tanzania kuwapa shule ya uongozi Makada nchi 6
Katika mkutano huo ameitaka kamati iliyowekwa kufanya kazi vizuri kama ilivyohimizwa na Umoja wa Mataifa na katika kauli mbiu ya siku ya watoto wa mitaani iliyoadhimishwa Tarehe 12 Aprili katika Kukuza Usawa na ubora wa huduma kutatua changamoto zao kitaalamu ili kuwajengea Maisha endelevu.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Zainab Chaula amesema ni jukumu la kila mmoja kutatua changamoto ya ukatili kwa wanawake na watoto.
Aidha amewataka wadau kukaa pamoja na kutafuta mbinu mbadala katika kutatua changamoto hii ili kuwaweka watoto wa kiume na wa Kike katika mazingira mazuri ya ukuaji na kujenga vijana wenye maadili na tamaduni za kitanzania