FINLAND imethibitisha Urusi kuikatia huduma ya umeme, Kampuni ya usambazaji wa umeme nchini Finland ya Fingrid imethibitisha kuwa hakuna tena huduma ya umeme kutoka nchini Urusi.
Naye Reima Paivinen, Makamu Rais wa Fingrid emesema walikuwa na uhakika wa kutokuwa na upungufu wa nishati ya umeme kutokana na kupatikana kwa usambazaji mwingine wa huduma hiyo kutoka nchini Sweden.
Huduma ya Umeme kutoka Urusi inakadiriwa kuchangia 10% ya nishati inayotumika na nchi ya Finland.
Umeme kutoka Urusi unachangia 10% ya umeme wote unaotumika nchini Finland
Kukatwa kwa umeme kunadaiwa kusababishwa na malipo kuchelewa kufanyika ingawa habari za kiintelijensia zinadai kuwa jambo hilo limechagizwa na hatua ya Finland kuthibitisha adhima yake ya kujiunga na Jumuiya ya Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (NATO).