Vigogo Yanga Wavamia Kambi..Wakimbia Mji wa Mwanza na Kujificha Huku



YANGA imebakiza pointi tatu kutangaza ubingwa baada ya juzi kutoa sare ya bao 1-1 na Biashara United sasa kilichopo mbele yao ni dabi ya Jumamosi dhidi ya Simba kwenye nusu fainali ya Kombe la Azam Shirikisho.

Jopo la kimkakati la viongozi wa Yanga limetua kambini kuongeza nguvu kwaajili ya mchezo huo ambao Kocha Msaidizi, Cedric Kaze amesisitiza kwamba maandalizi yake yatakuwa ya kipekee.

Mwanaspoti linajua kwamba viongozi waliotua kambini ni Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Hersi Said na msaidizi wake,Rodgers Gumbo pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu, Senzo Mazingisa.

Kikawaida viongozi hao ni adimu kukutana kambini lakini Hersi amesisitiza kwamba kwa hali ilivyo lazima wakaze kila kona kwani Jumamosi wana jambo zito na la heshima kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.


Hersi alisema baada ya kukaa Mwanza siku tatu wameona walikimbie jiji hilo na kwenda kukaa umbali wa kilometa 151.7 mkoani Shinyanga ambako kila kitu kiko sawa na ulinzi utaboresha zaidi.

Ameliambia Mwanaspoti kuwa wamefikiria mambo mengi katika kuchukua uamuzi huo lengo likiwa kuwapa utulivu wa akili wachezaji wao kabla ya mechi hiyo kubwa.

“Mwanza ni pazuri lakini unajua hii ni mechi kubwa na muda unavyosogea watu watazidi kufika hapa kwahiyo tunataka kuona wachezaji wanakuwa kwenye utulivu wa akili,”alisema Hersi ambaye alisisitiza kwamba watafanya maandalizi ya kina na tofauti zaidi.

“Tumeona Shinyanga ni muafaka kwetu tutapata sehemu nzuri ya kufanyia mazoezi lakini pia hakutatupa ugumu wala kuwachosha wachezaji wakati tukitaka kurejea hapa,”alisema na kuongeza kuwa Yanga ilishasafirisha kundi kubwa la walinzi wake wakiwagawanya katika makundi mawili nusu wakibaki jijini Mwanza na wengine wakipelekwa Shinyanga katika eneo ambalo wataweka kambi hiyo fupi.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Mashindano Rodgers Gumbo alisema kila kitu kinakwenda sawasawa katika hesabu zao na kwamba wako kamili kwa ulinzi na mazingira yoyote ya kukabiliana na ugumu wa mchezo huo.

“Tupo sawasawa unajua Yanga inapokwenda kokote ina ulinzi mkubwa wako watu wetu lakini pia hujumuika na wenzetu wenyeji ambao tunakutana nao kokote tunakokwenda kwahiyo maandalizi yetu ni makubwa sana,”alisema Gumbo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad