Bia nchini Afrika Kusini zinatajwa kuuzwa kwa wingi kuliko vinywaji baridi visivyo na vileo hii ni kwa mujibu wa wachambuzi wa data za watumiaji katika kampuni ya NielsenIQ SA.
"Tumefuatilia mauzo katika maduka zaidi ya 150,000... iwe ni maduka rasmi, migahawa, vioski," msemaji aliambia shirika la habari la eNCA.
Ripoti ya Kampuni hiyo inasema mauzo ya bia nchini Afrika Kusini yamepanda kwa 8% katika kipindi cha miezi 12 iliyopita
Alipoulizwa kuelezea ongezeko hilo, Jon-Jon Emary wa NielsenIQ SA alisema "ukuaji mkubwa" umekuja "kufuatia marufuku mfululizo tulizoona wakati na baada ya sheria ya kutotoka nje tuliyokuwa nayo 2020".