Wabunge wacharuka kiingereza kitumike kufundishia ‘tutapigwa goli’



MJADALA kuhusu lugha gani itumike kufundishia kati ya kiingereza au Kiswahili umeendelea kutikisa baada ya asilimia kubwa ya wabunge kushauri kuwa kiingereza kitumike kwani Tanzania sio kisiwa.

Pia wameshauri badala ya kulikimbia tatizo la kutokuwa na walimu wenye uweledi wa kufundisha kwa lugha ya kiingereza, walimu hao nao wanolewe ili wapatikane walimu stahiki. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma… (endelea).


Prof. Ndakidemi
Hayo yamebainishwa leo tarehe 7 Mei, 2022 jijini Dodoma katika Mkutano wa kupokea maoni ya wabunge juu ya maboresho ya sekta ya elimu na mabadiliko ya mitaala ya elimu ya msingi.

Akichangia maoni katika mkutano huo, Mbunge wa Moshi Vijijini ,Profesa Patrick Ndakidemi (CCM) amesema Tanzania isipotumia kiingereza watanzania watapata tabu kupata ajira nje ya nchi.


 
“Kuhusu lugha ya kutumia nitakuwa mkweli, mfano tukisema tunakwenda na kiswahili moja kwa moja ilihali hatutajiandaa kuwa na maneno kamilifu ya kiswahili kwenye sayansi, ukitoka hapa na kiswahili chako ukienda Kenya, Uganda au pengine utabaki hapohapo Tanzania.


Prof. Mkumbo
“Mawazo yangu kuhusu lugha ni kwamba lugha ya kiingereza inatumika duniani kote, hivyo tuipe kipaumbele la sivyo tutakapotoka hapa kwenda kwa wenzetu tutapigwa goli,” amesema.

Amesema Wakenya wanawazidi Watanzania katika sokon la ajira kwa sababu wanajua kiingereza.


“Wakienda huko kwingine wanapewa kipaumbele, kwa hiyo tuhimize kiingereza kitumike na Kiswahili kitumike pale panapostahili,” amesema.

Hoja ya Prof. Ndakidemi imeungwa mkono na Mbunge wa Viti Maalumu –CCM, Shari Raymond ambaye amesema watoto wa zama hizi hawaijui lugha mama (lugha za makabila) zaidi ya Kiswahili hivyo ni vema wakafundishwa kwa kutumia kiingereza.

“Bado hatujafikia wakati wa sisi kutumia lugha yetu Kiswahili kufundishia masomo, kiingereza kipewe kipaumbele tena kianze kutumika kuanzia darasa la kwanza,” amesema.

Aidha, Mbunge wa Singida Kaskazini, Ramadhan Ighondo (CCM) alipingana na hoja za Prof Ndakidemi pamoja na Shari na kudai kuwa lengo la kumpeleka mtoto shule ni kuboresha maarifa, sio lugha.


 
“Utafiti niliofanya ni kwamba watoto wetu wanapotoka shule ya msingi wanatoka wakiwa na uelewa lakini wakifika sekondari wanakunja sura.

“Tatizo sio watoto wakajue lugha, tunataka wakapate maarifa, wakienda China wanajifunza kwanza kichina ndipo wajifunze udaktari, Urusi na Japan vilevile, tuondoe boriti kwamba kiswahili ni lugha masikini…tuweke watalaam, watafsiri misamiati ya kisayansi,” amesema.

Wakati Mbunge wa Ubungo, Prof. Kitila Mkumbo kwa upande wake ametolea mifano nchi za Asia kama vile Singapore kuwa inatumia kiingereza na kufanikiwa kukua kiuchumi.

Amesema badala ya kulikimbia tatizo ni vema kulitibu kwa maana kuwa kama hakuna walimu wa kingereza, wafundishwe na kupatikana walimu stahiki wa kufundisha lugha hiyo.


Hata hivyo, alienda mbali zaidi na kuishauri Serikali iondoe kodi kwa wamiliki wa shule binafsi ili wajitokeze wengi kufungua shule nyingi na kupunguza uhaba wa ajira za walimu nchini.

Awali akifungua mkutano huo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda leo Jumamosi amesema hadi kufikia Disemba mwaka huu atahakikisha rasimu ya maboresho ya sera na mitaala yake imepatikana wakati kufikia Januari mwaka 2023 wataanza mchakato wa kupata idhini serikalini.


Prof. Mkenda
Amesema kwa vyovyote dunia ina msukumo wa mageuzi ya elimu ndio maana Shirika la Fedha Duniani (IMF) linataka kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa nchi zinazofanya mageuzi kwenye elimu.

Vilevile katika mkutano wa wadai wa elimu uliofanyika hivi karibuni Doha nchini Quatar umeonesha kuwa kuwa kutakuwa na msamaha wa madeni kwa nchi ambazo zitakuwa na mageuzi makubwa ya elimu.

“Kwa vyovyote vile mageuzi ambayo tunakwenda nayo yatakuwa makubwa katika historia ya nchi yetu hatutaki kubahatisha, kukurupuka ndio maana tunahitaji sana kusikiliza maoni yenu wabunge,” amesema Prof. Mkenda.


 

 

+255-067595****
2min

Wanaosema mtu anaelewa kwa lugha yake wao wenyewe walitumia kiingereza hivi hawakuelewa chochote? tatizo limeanza sasa tujiulize kimetokea nini. mbona wazee wetu walioleta uhuru walikuwa wasomi wazuri akina Nyerere Nkuruma Mugabe na wale ambao hawakuwa viongozi waliosoma zamani ni bomba. kama walivyosema wenzangu tusikimbie tatizo. tulitatue. mngefanya research muone kwa miaka miaka mingi wanafunzi walifeli kiswahili kuliko kiingereza hata leo hata kiswahili kwao ni tatizo. tujiulize kimetokea nini badala ya cheap answers tuaingia kosa la mwaka kama tulivyokwishakosea kt mengi huko nyuma. wanaosema hivyo watoto wao wapo English medium au nje ya nchi na wao wanaenda popote duniani wanataka kukwamisha wengine. basi iwe hiari ya mtu tusilazimishane sababu kila moja na mipango na maisha yake hutanipa ajira weweZaidi


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad