Wanafunzi 76 wa Shule ya Sekondari ya Wasichana Mkuza Kibaha Mkoani Pwani wamenusurika katika ajali ya moto iliyotokea usiku huu katika bweni la Shule hiyo na kuteketeza mali za Wanafunzi hao ikiwemo nguo,madaftari pamoja na vitabu "Moto huo umetokea wakati Wanafunzi wapo kwenye Ibada hivyo hakuna Mtoto yeyote aliyepata madhara"
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amefika katika eneo la tukio na kuwatoa hofu Wazazi wasiwe na shaka kwani Watoto wako salama na wameshapata mahali pa kuhifadhiwa, mpaka sasa tayari imeundwa Timu kwa ajili ya kuchunguza tukio hilo.
Kamanda wa Zimamoto Mkoa Pwani, Jenipher Shirima amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo na kutoa rai Kwa Wananchi kutoa taarifa Kwa wakati Ili kudhibiti moto au kupunguza athari za moto pindi unapotokea.
Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT (Wamiliki wa Shule hiyo), Dr. Alex Malasusa ameushukuru Uongozi wa Mkoa wa Pwani pamoja na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kwa ushirikiano wao katika tukio hilo.