Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro Ngollo Malenya ameonya baadhi ya watu ambao wamekuwa na tabia ya kurekodi matukio katika ajali badala ya kupiga Simu jeshi la zimamoto na kusabisha madhara makubwa kwa Wananchi.
DC Malenya ametoa onyo Hilo wakati akifunga kilele Cha maadhimisho ya Zimamoto mkoani Morogoro ambapo amesema kumekua na tabia sio ya kizalendo ya watu kupiga picha majeruhi,au maiti katika matukio ya ajali na kuyasambaza katika mitandao ya kijamii huku wao wakiwa hawana taaluma ya habari hivyo wametakiwa kuacha mara moja kwani Jambo Hilo Ni kinyume na maadili na sheria za mitandao ya kijamii.
Kwa taarifa zaidi unaweza ukabonyeza play kufahamu zaidi.