Watu watatu wameua na Tembo katika kijiji cha Kilosa kwa Mpepo wilayani Malinyi mkoani Morogoro
Watu hao walikuwa wakielekea shambani ambapo kundi la wanyama hao lilivamia kijijini hapo na kusababisha mauti ya watu hao
Wakizungumza na EATV ndugu wa marehemu wanasema kuwa nduzu zao wamekutwa na mauti wakiwa wanaelekea shambani
Waliopoteza maisha ni Colletha Gimwalasa, Geoffrey Sawasawa na mwingine ambaye hakufahamika mara moja jina lake mara moja
Wanasema changaamoto ya uvamizi wa wanyama hao imekuwa ni ya muda mrefu huku jitihada za kukabiliana nao zikikwama mara kwa mara kutokana na ukosefu wa mawasilinao baina yao na mamlaka ya usimamaizi wa wanyama pori
Wakizungumza katika mazishi ya watu hao wahifadhi kutoka TAWA wanewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kuiomba serikali kuharakisha upatikanaji wa mtandao wa simu wa uhakika, kujengwa vituo vya ulinzi, pamoja na kurekebishwa baadhi ya barabara za kufika eneo hilo ili kuweka uharaka wa upatikanaji huduma sambamba na uokoaji pindi yanapotokea majanga ya namna hiyo