Watumishi wa Sekta Binafsi nao Mbioni Kuongezewa Mishahara

 


Mwenyekiti wa Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya (TUGHE) taifa bwana Joel Kaminyoge amesema watumishi wa sekta binafsi watarajie kucheka wakati wowote kabla ya tarehe moja mwezi wa saba kutokana na bodi ya kima cha chini cha mishahara kwa sekta binafsi kuelekea mwishoni mwa ukamilishaji wa zoezi la upangaji wa mishahara.


Kaminyoge amebainisha hayo mkoani Njombe alipokuwa kwenye ziara yake ya kawaida ya kuimarisha Chama alipokutana na watumishi ambao ni wanachama wa chama hicho katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe.




“Upandishwaji wa mishahara umefanywa kwenye sekta ya umma,wakati wowote kabla ya tarehe moja july watumishi kutoka sekta binafsi na wenyewe watacheka na hii ni kwasababu kuna bodi mbili za kima cha chini cha mshahara,hii sekta ya umma imeshafanya ndio maana Rais ametangangaza hii sekta binafsi bado wanaendelea kufanya wakati wowote tutasheherekea kwa pamoja”alisema Joel Kaminyoge

Dkt,Apolinary Nombo ni mwenyekiti wa TUGHE tawi la hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe ameishukuru serikali kwa kupandasha kima cha china cha mshahara kwa 23.3% kwa kuwa imekwenda kuongeza ari kwa wafanyakazi.


“Tunaishukuru serikali kwa kuongeza hiki kiwango kwa kuwa Mh Rais ametengeneza ari mpya kwa watumishi na kufanya kazi kwa juhudi zaidi”alisema Dkt.Nombo


Baadhi ya wanachama wa Chama hicho ambao ni watumishi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe akiwemo Bariki Mwambije na Neema Hyela wameshukuru Chama hicho kwa kuendelea kupambania haki za wafanyakazi huku wakizidi kuomba vyama vya wafanyakazi kuzidi kupambana na unyanyapaa wa watumishi katika ofisi zao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad