Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa 'Wanafunzi 14,254 Wamekosa Nafasi"

 


Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa leo amesema "Kwa kuangalia takwimu za mwaka 2022, kumekuwa na ongezeko la Wasichana 7,555 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na Vyuo vya Ufundi ukilinganisha na mwaka 2021, hata hivyo idadi hii bado ni ndogo kulinganisha na Wavulana, ili kukabiliana na changamoto hii, Wizara inaendelea kuboresha miundombinu ya Shule ili kuhakikisha Wasichana wengi zaidi wanajiunga na kidato cha tano, aidha, tunachukua nafasi hii kumshukuru Rais Samia kwa kuwezesha ujenzi wa Shule za Wasichana kumi za mikoa ambapo kila Shule itachukua Wanafunzi wapatao 300 kuanzia mwaka 2023"


"Pamoja na kuwepo kwa ongezeko la Wanafunzi waliojiunga na kidato cha tano, Vyuo vya Ualimu na Vyuo vya Elimu ya Ufundi kwa mwaka 2022, jumla ya Wanafunzi 14,254 wakiwemo Wasichana 3,901 na Wavulana 10,353 wamekosa nafasi, kati yao, Wanafunzi 12,876 wana sifa ya kujiunga na kidato cha tano, hali hii imetokana na ongezeko kubwa la Wanafunzi waliofaulu na waliokuwa na sifa ya kujiunga na kidato cha tano na Vyuo vya Ufundi pamoja na ufinyu wa nafasi za kidato cha tano na Vyuo vya Elimu ya Ufundi (NACTVET)"


"Wanafunzi hao wanatarajiwa kujiunga na kidato cha tano katika awamu ya pili baada ya ukamilishaji wa baadhi ya miundombinu ya Shule na Vyuo"

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad