ZA NDAANI KABISA: Wanne kupigwa panga Simba...



MABOSI wa Simba bado hawajaweka wazi kuanza mchakato wa usajili kwa maana ya majina ya mashine mpya ambazo watazileta kwa ajili ya kuongeza makali pamoja na wale watakaowaacha.

Wiki hii inayomalizika leo kumekuwa na vikao vingi vya siri kubwa na lengo kubwa likiwa ni mipango ya msimu ujao na kuanza harakati za usajili ili kupunguza presha pindi dirisha la usajili litakapofunguliwa.

Za ndaani wiki hii inafahamu mabosi wa Simba wamepanga kuwaacha wachezaji wa kigeni sio chini ya wanne na nafasi hizo kuzibwa na mashine mpya zitakazoingia nchini kabla ya msimu ujao kuanza.

Miongoni mwa mashine hizo mpya tayari mabosi wa Simba wamekamilisha dili la mshambuliaji wa Zanacco, Moses Phiri ambaye atakuja kuchukua nafasi ya Bernard Morrison aliyeonyeshwa mlango wa kutokea.


 
Nyota wengine wa kigeni waliokuwa katika wakati mgumu ni beki wa kati, Pascal Wawa anayemaliza mkataba na Simba mwisho wa msimu huu.

Kinara wa mabao kwenye kikosi cha Simba hadi sasa akiwa amefunga nane kwenye Ligi Kuu Bara, Meddie Kagere naye amekalia kuti kavu na mwisho wa msimu huu mkataba wake unafikia ukingoni. Wakati huo huo kuna mvutano kwa mabosi hao dhidi ya wachezaji watatu, Peter Banda, Chris Mugalu na Rally Bwalya.

Mugalu mwisho wa msimu huu mkataba wake unamalizika ila kocha wa Simba, Pablo Franco mbali ya majeraha ya mshambuliaji huyo amekuwa akivutiwa naye.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad