Zitto Autaka Urais, Agusia Uwezekano wa Vyama vya Upinzani Kuungana



KIONGOZI wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe ameweka bayana kuwa anatamani kuwa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania siku moja kwani anaamini anao uwezo wa kuwatumikia wananchi kutokana na uzoefu alionao katika siasa lakini pia maarifa.

“Nimesema siku zote kwamba urasi nautaka, siwezi kusema moja kwa moja kwamba nitagombea mwaka 2025, kwasababu uamuzi huo unatokana na kwanza kudra za mungu na pia Chma na wananchi ambao ndiyo lazima watoe ridhaa na dhamana ya kuiongoza nchi katika nafasi hiyo.” Alisema Zitto


Zitto Kabwe anautaka Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Kiongozi huyo amegusia suala la kuitoa madarakani CCM kuwa siyo jambo rahisi na ili kukamilisha lengo hilo Vyama Vya Upinzania havina budi ya kuungana na kusimamisha mgombea mmoja amabaye ataweza kupambana kuhakikisha CCM inatoka madarakani.

Zitto pamoja na viongozi wengine wa Chama cha ACT- Wazalendo wameweka kambi ya zaidi ya mwezi mmoja mkoani Mwanza ambako wanafanya kampeni ya kuimarisha chama.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad